DALILI ZA HOMA YA MATUMBO (fowl typhoid)

 DALILI ZA HOMA YA MATUMBO (fowl typhoid)

1.Kupoteza hamu ya kula 

2.Kupunguza kutaga 

3.Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano 

4.Manyoya ya kutimka , kushusha mabawa , kufumba macho na kuzubaa (kuvaa makoti)

5.Kupauka kwa upanga na masikio sababu ya kupungukiwa damu 

6.Vifo kutokea kidogokidogo na KUNDI lisilotibiwa hufikia 50%

DALILI KWA VIFARANGA 

1.Kuanguliwa vikiwa dhaifu na kushindwa kutembea 

2.Kujikusanya pamoja na kukosa hamu ya kula 

3.Kinyesi cha rangi ya njano na huganda kwenye manyoya sehemu ya kutolea haja 

4.Kupumua kwa shida 

Soma na hii

Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1

DAWA ZA MAFUA YA KUKU (infection coryza)

1.Fluban

2.Ganadexil

3.Tylodox

4.Teramycin 

NB: Tumia fluban kwa kuku wanaoonesha dalili za mafua bila vifo

Tumia tylodox/ganadexil kwa kuku wenye mafua na tayari kuna vifo vimetokea  

MAHEPE (MARECK'S DISEASE) 

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku wa mayai  

ndio wanaoathirika zaidi. Mara nyingi ugonjwa hutokea katika kuku wenye umri kati ya wiki 12 hadi 24, ijapokuwa  hata kuku wakubwa nao hupata ugonjwa. Huu ni ugonjwa unaowapata kuku, ambao unasababishwa na kirusi aina ya "HERPES VIRUS".

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea 

•  Maambukizi pia kuenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda na vumbi  

litokanalo na manyoya.  

•  Mate ya kuku wagonjwa pia ni njia mojawapo ya maambukizi 

•  Binadamu, inzi na aina nyingine za ndege pia zinaweza kusambaza maambukizi.

Soma na hii

Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1

Dalili za Ugonjwa wa Mahepe (Mareck's Disease)

Dalili 

•  Uharo mweupe wenye maji maji  

•  Mboni ya jicho kuwa na rangi ya kijivu 

•  Upofu kwenye kuku  

•  Miguu na mabawa hupooza  

•  Kuku kupindisha kichwa  

•  Kwa kawaida vifo ni kati ya asilimia 10 na 80.

Uchunguzi wa Mzoga 

•  Uvimbe mweupe karibu katika viungo vyote laini vya mwili: maini, figo, bandama na ngozi. 

•  Mishipa ya fahamu kuvimba katika miguu na mbawa zilizopooza

Kuzuia na Kinga 

•  Mizoga, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au kuzikwa. 

•  Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa 

•  Baada ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa 

•  Hakikisha unatenganisha kuku wadogo na wakubwa hadi miezi 3, na watenganishe kuku kwa umri 

•  Vifaranga vya siku moja vipatiweRelated  Chanjo dhidi ya ugonjwa 

Tiba:

Hakuna matibabu yaliyogundulika kisayansi, ila kama ugonjwa huu umeingia katika mifugo yako tenganisha wazima na wagonjwa kuku wapatiwe chakula cha kutosha na vitamini muda wote

Soma na hii

Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us

Most Popular

Popular Posts