Mmea wa Azola. Huu ni mmea ambao hukua ndani ya muda mfupi na uweza kulisha mifugo yako (kuku, ng’ombe, nguruwe, bata, samaki n.k) na kuwapatia chanzo kizuri cha protini pamoja na viini lishe vinginevyo.
MAZINGIRA YA UZALISHAJI
• Eneo ambalo litatumika hakikisha lina funikwa vyema kuweza zuia upotevu mkubwa wa maji, na kuchanganyana na uchafu wa aina yeyote.
• Eneo lisiwe na shughuli nyingine kuepuka kuchanganyikana na uchafu mwingine pamoja na sumu zingine.
• Eneo liwe na uhakika wa maji kwa kipindi cha mwaka mzima.
JINSI YA KUOTESHA
• Andaa bwawa kulingana na uwezo ulio nao na idadi ya mifugo unayotaka kulisha. Kina cha bwawa lako kiwe ni sentimita kumi na tano (15)
• Kisha weka nailoni ngumu au turubahi ambalo lituzuia kupotea kwa maji Kunywea chini. Baada ya hapo weka mchanganyiko wa samadi na udongo kwa uwiano sawa kujaza kina kwa sentimita. Baada ya hapo weka maji ili kujaza sentimita sita za juu. Ondoa uchafu wote utakao jitokeza baada ya kuweka maji juu ya mchanganyiko wa udongo na samadi.
• Mimina mbolea ya maji aina ya EMO kwa uwiano (Mils 20: lita kumi za maji). Hapa utahitaji kujua ukubwa wa bwawa lako ili kuelewa ni kiasi gani cha mbolea kinatakiwa kwenye bwawa lako.
• Kisha weka mbegu ya Azolla juu ya maji hayo kwa kusambaza sehemu mbalimbali.
• Baada ya azolla kuota subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka. Anza kuvuna na kuwapatia mifugo yako.
Azola hujizalisha kwa haraka sana kwani ndani ya siku 2 au tatu mmea huu hujizalisha mara 3 au nne zaidi. Hivyo bwawa dogo la ukubwa wa mita za mraba kumi (10 M2) linaweza kuwa mkombozi kwa wafugaji wadogowadogo
NAMNA YA KUWALISHA.
Kuna namna mbili kuu za kuwalisha mifugo
1. Namna ya kwanza kwa kuwapatia kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani au ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100. Hapa mifugo inatofautiana uchanganyaji.
2. Namna ya pili kwa kuwapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine. Kinafaa kwa kuwa kina virutubisho vingi ila kwa mara ya kwanza yafaa kuchanganya kwa sababu mifugo inakuwa haijakizoea.
MATUMIZI YA ZIADA YA AZOLLA
• Kama mbolea mashambani / Bustanini: Weka Azolla ardhini ioze huko huko; utakuwa umeweka virutubisho vya kutosha kwa ajili ya mimea.
• Mazingira: Huonndoa hewa chafu angani na pia hutakatisha maji.
• Hutumika kutengeneza mafuta ya magari na vilainishi.
• Hutumika kuzalisha mafuta ya ndege
• Hutumika kuzalisha dawa za hospitalini.
• Habari njema ni kwamba kuna aina tisa za azola lakini mbili kati ya hizo zinapatikana Tanzania tu. Hivyo ni fahari kujivunia kuishi Tanzania kwani kuna vitu vingi vya kipekee.
Post a Comment