UTENGENEZAJI WA FUNZA KAMA CHAKULA CHA KUKU
🐓🐔Moja ya virutubisho muhimu vya kuku ni protini ambayo unaweza kuwapa kupitia vyakula mbalimbali. Funza ni wadudu walio na protini nyingi ambayo inahitajika sana kwa ajili ya ukuaji wa kuku. Zipo njia mbalimbali ambazo zinatumika kutengeneza funza na hivyo kupunguza gharama za vyakula vya kuku.
🐣HATUA ZA KUTENGENEZA FUNZA
🐛1. Tafuta kinyesi cha kuku au mavi ya ng'ombe ambayo unaweza kuyapata machinjioni au toka kwa kuku wako mwenyewe.
🐛2. Chukua kinyesi weka kwenye kidumu kilichokatwa kisha weka pumba za mahindi kwa juu.
🐛3. Kisha weka maji kidogo ili kuvutia nzi waweze kutaga mayai. Utaendelea kuweka maji hapo kwa siku 2 na kisha uache siku ya tatu, siku ya nne au tano funza wataanza kutokea.
🐛4. Wakusanye funza waliozalishwa kwenye kidumu chako.
🐛5. Waoshe na kisha wape kuku wako wale
🐔🐓FAIDA ZA FUNZA:
FUNZA ni mdudu aliebarikiwa kuwa naprotini nyingi sana kwa kuku pia humfanya kuku kunawiri na kuongeza kasi kasikidogo ya kutaga ni mdudu ambaye kuku akimuona humtamani wakati wowote😋.
Post a Comment