UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER) HATUA KWA HATUA

UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER) HATUA KWA HATUA


Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shambal mahali unapotaka kufugia ni kama inavyoonyesha hapa. 


Mazingira yanayolizunguka banda la kuku na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.


Hakikisha sehemu ya kulelea vifaranga (brooding area) inawekewa chanzo cha joto saa moja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya eneo la kulelea vifaranga


Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga wafikishe kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe glucose na baada ya hapo chakula.


Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye kiti cha gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka msongo (stress)

Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1

Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10 chicks/1m square) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.


Mambo ya kuzingatia baada tu ya vifaranga kufika bandani (MAIN TIPS)


Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye boksi mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.


Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa 23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.


Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamini kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.


4. Hakikisha unapanga vyema vyombo vya chalula (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila ya kupata shida.


JOTO


Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na chanzo cha joto, au angalia tabia za vifaranga wako ndani ya banda


2. Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya nyuzi joto 30-35. Njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo yako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto.


Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.


Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35.


MAJI


Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihabarishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. Kuku kutokunywa maji ni kielelezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida. Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 (vyombo vya maji) kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.


CHAKULA


Chakula kinapaswa kuwekwa katika visahani maalumu vya kulishia vifaranga kwa muda wa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula kwenye vyombo maalumu vya kulishia kuku (feeders). Kwa kawaida inashauriwa kuweka vyombo 4 vya chakula kwa vifaranga mia moja, na hii inafaa itoshe eneo la asilimia 50 tu katika eneo la kulelea vifaranga (brooder). Kwa feeder za kawaida inashauriwa/ inapaswa kuwa feeders 3 -4 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na Mwanga, Maji na Panya.


Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi. Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa 8 kisha masaa 24 kama wamekula na hii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume cha hapo inaonyesha hawajala.

Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1

AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA:


Chakula cha vifaranga (Super starter) Vifaranga wapewe kilo 0.5 ya chakula kwa kila kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa vidonge (pellet) kama unabuwezo wa kupata (pette) na kama huna uwezo huo wapatie starter ya kawaida kwa muda wa wiki 2 au unaweza kufuata mfumo wa kawaida wa ulishaji. Chakula cha kuku wanaokua (Grower) Kuku nwanaokua wapewe kilo 1.5 ya chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa vidonge (pellet) kwa muda wa wiki 2 au unaweza kufuata ratio ya mfumo wa kawaida au bila kuwapimia.


Kuku wakubwa (Finisher):

Kuku wa hatua hii wapewe kilo 1.5 ya chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza na hapo unaweza kuwauza siku yoyote.


MAMBO MUHIMU KWA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA KULINGANA NA UMRI WAO MFUMO WA KWANZA:


SIKU 1-5


Wapewe glucose na mchanganyo mmoja wapo kati ya hii ifuatayo


Neoxyvital au OTC plus na typhorium au trimazine


Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte.


CHAKULA


Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.


SIKU YA 6


Vitamini (vitastress)


SIKU YA 7


Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress) 


WIKI YA PILI


Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)


WIKI YA TATU


Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7.


WIKI YA NNE:


Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)


WIKI YA TANO


Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)


WIKI YA SITA:


Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni - Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili


NB: SIO LAZIMA KUWAWEKA KUKU WAKO MPAKA WEEK YA 6 FUGA KUTOKANA NA UHITAJI WAKO, WATEJA UNAOWAPATA NA WATU WANAOKUZUNGUKA. WENGI WETU HUFUGA SIKU 21-30 KULINGANA NA UHITAJI.


MFUMO WA PILI:


Ni huu wa kawaida ambao ni kufuata ratiba ya kawaida. Lakini inatakiwa tu kuwa makini Na huu mfumo kila mtu anaufahamu kama hivi.


Broiler huwa wana aina mbili za ulishaji.


Kuanza (supper starter) na kumaliza (finishers)


Kuanza (starter), kukuza (growers) na kumalizia (finishers)


KWANZA


Aina ya kwanza huwa ni wiki 2 za mwanzo hupewa chakula cha kuanzia (Supper starter) na wiki mbili zinazofuata mpaka kuuzwa hupewa chakula cha kumalizia (broiler finishers)


 PILI


Aina ya pili huwa chakula cha kuanzia wiki 2 za mwanzo (supper starter) chakula cha kukuzia (broiler growers) wiki ya 3 na chakula cha kumalizia (broiler finishers) wiki ya 4 hadi kuuzwa

Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us