MFAHAMU KUKU WA ASILI (pure chicken)
Kuku wa asili ni wale ambao damu yake aijachanganyika na kuku wa kigeni
Wana rangi na maumbile mbali mbali na inakadiliwa kuwa hapa tanzania kuna kuku wa ASILI zaidi million 58
Soma na hii
Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1
SIFA ZA KUKU WA ASILI
Kuku hawa hutoa mazao machache kwa maana ya nyama na mayai
Kuku wa asili utaga mayai 40-60 ndani ya mwaka mmoja , badala ya 100-150 Iwapo atatunzwa na kulishwa vizuri
Vivyo hivyo uzito wa kuku wa asili huko chini zaidi
Wastani wa kilograms 1.0 - 1.5 badala ya 1.8 - 2.5 Iwapo atatunzwa na kulishwa vizuri
Wastahimilivu wa magonjwa lakini Ni vema uwape CHANJO (vaccine)
Wana uwezo wa kujitafutia chakula wenyewe , Ila ni vema uwape chakula bora cha ziada
Wana uwezo wa kuatamia mayai , kutotoa na kulea vifaranga katika mazingira magumu
Vile vile Wana uwezo wa kujilinda na kulinda vifaranga dhidi ya adui Kama(defense mechanism)
Nyama na mayai vina radha nzuri kuliko kuku wa kisasa
Soma na hii
Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1
MFAHAMU SASSO
Sasso ni Aina ya kuku vile vile ni brand name ya kampuni kubwa ya kuku iliyopo ufaransa ilianzishwa mwaka 1978
Sasso ni free range chicken , unaweza kuwafuga huria na wanauwezo wa kujitafutia chakula chao wenyewe
Sasso ni coloured brees sababu Wana rangi mchanganyiko na ata vifaranga vyao uwa na rangi tofauti
Wanauwezo wa kutaga mayai 150+ na kuendelea kwa mwaka ikiwa utawalisha vizuri
Ni kuku wanaotumika kwa mayai pamoja na nyama , uanza kutaga kuanzia miezi 5 - 6
Tetea anaweza kufikisha uzito wa kilograms 3.5 hadi 4 Kama akilishwa vizuri
Jogoo anaweza kufikisha uzito wa kilograms 4.5+
Soma na hii
Post a Comment