JE UNAJUA UMUHIMU WA VITAMIN KWA KUKU🐓?
UKOSEFU wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin.
📌 UMUHIMU WA VITAMINI.
- Husaidia katika ukuaji wa kuku.
- Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka.
- Husaidia kuku kuwa mwenye afya.
- Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri.
📌 UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU
Ukosefu wa vtamin 'A' hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin 'A' kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa kwa ukosefu wa vitamun 'A' pia hata kuku wakubwa.
Soma zaidi
Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1
📌 DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU
-Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji
-Hudhoofika na hatimaye kufa na kuku ufa kwasababu uwa ni kipofu na hawezi kuona chakula kwahyo kuku ufa kwa njaa
📌 TIBA NA KINGA
-Kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani
-Wape kuku vitamini za kuku za dukani kama TOPVITA kwasababu Topvita ina muunganiko wa vitamin ya A, D, E, B/ COMPLEX - C
-Kwa kuku alie athirika na ugonjwa huu msafishe na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi hakikisha uchafu wote unatoka kisha mpe vitamin ya dukani kama FARMVITA, LAY VITA, TOPVITA au STRESS VITA Fanya zoezi hilo kwa siku 5.
📌 VITAMINI B
Manyoya huonekana kusambaratika, panga za kuku kuonekana zikiwa zimepauka, na kwa kuku watagaji hupunguza uwezo wao wa kutotoa mayai.
Soma zaidi
Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Wapatie kuku wako Dawa za multivitamin kama TOPVITA A,D,E,B,/COMPLEX -C
📌 VITAMIN E
Hizi ni dalili za ukosefu wa vitamin E kwa kuku,
- shingo huanguka chini na kupinda.
- Vifaranga huanguka kifudi fudi.
- Utagaji wa kuku hushuka kwa kiasi kikubwa.
📌 VITAMIN D
Ukosefu wa vitamin D hupelekea tatizo la mifupa kuwa laini, na hali hii hupelekea mifupa kupinda pia magoti huvimba na hata midomo kuwa laini. Na hata ukuaji wa kuku huwa wa hafifu. Hii hutokana madini aina ya madini ya calcium na fosifolusi kutojengeka kwenye mifupa.
Kwa kuku watagaji hali hii hupeleka kwa kuku watagaji kutaga mayai yenye ganda laini.
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mimea, mfano majani ya lusina, mpapai, mchicha na mikunde
Kazi ya vitamini ni kulinda mwili dhidi ya magonjwa, ila unaweza kutumia madini ya selenium kuongezea kwenye chakula cha kuku au unaweza kutumia STRESS VITA , FARMVITA au TOPVITA A, D, E,B,/COMPLEX -C
Soma zaidi

Post a Comment