DRUGS RESISTANCE (usugu wa madawa)
Kwa mujibu wa tafiti MBALIMBALI tatizo ili la(drugs resistance) limekua likiongezeka siku baada ya siku
CHANZO CHAKE
Kila dawa (drugs) anayopewa mnyama inakua na muda wa kukaa na kupotea mwilini kitaalamu wanaita withdrawal period
Kuna baadhi ya dawa kama zile zinazoua bacteria zikitumika ubakia mwilini kwa muda tofauti
Ikiwa utatumia dawa yenye kiwango kikubwa usababisha vimelea vya ugonjwa husika kuwa sugu na kutosikia dawa
Upelekea ata kama utatumia dawa ya aina hiyo haitafanya kazi , utalazimika kutumia dawa nyingine
Vile vile kutumia dawa Isiyo sahii upelekea kukomaza vimelea vya ugonjwa husika na kusababisha kutosikia dawa
NB : Hutakiwi kutumia dawa zenye dozi kubwa kabla ya kuanza kutumia dawa zenye dozi ndogo
Kwa mfano ikiwa kuku wako ndio anaanza kuumwa mafua , usikimbilie kutumia dozi kubwa kama enrovet au limoxin
Ni vema ukaanza na FLUBAN
Madhara yake ni kwamba ikishindwa kutibu itakuleta ugumu kupata mbadala wa dawa ya kutibu mafua makali
Vile vile swala la kuchanganya madawa bila kujua zina faa kuchanganywa au lah
Ni vema upate ushauri kwa doctor kabla ya kuanza kuchanganya
Pia usiwape kuku wako madawa ikiwa awana ugonjwa wowote , uchangia kuku kupata tatizo la USUGU WA DAWA
Post a Comment