JINSI YA KUPAMBANA NA KIDERI(NEWCASTLE)
Ugonjwa wa kideri au kwa lugha ya kitaalamu unafahamika kama Newcastle disease husababishwa na virusi ambavyo vimeenea duniani kote na hushambulia kuku wa rika mbalimbali. Ugonjwa huu husababisha vifo vingi haswa kwa vifaranga.
Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1
DALILI :
Dalili za wazi za ugonjwa ni:
• Idadi kubwa ya vifo vya ghafl a kwa kuku wa rika zote
• Kupungua kwa uzalishaji wa mayai na nyama (asilimia 30-50 au pengine zaidi)
• Kutaga mayai yenye magamba membamba
• Kuku kukohoa na kushindwa kupumua
• Kutokwa na ute mzito mdomoni
• Kupinda shingo
• Kuharisha mharo wa kijani
UCHUNGUZI BAADA YA KIFO:
• Mzoga wa mnyama anapopasuliwa koromeo na utumbo huonekana kuwa na damudamu (petechial haemorrhage) na pia kwenye fi rigisi na katika kiungo kabla ya firigisi (proventiculus).
Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1
MASHAMBULIZI YA KIDERI
MAAMBUKIZI:
Virusi vya kideri husambazwa haraka toka kuku mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kinyesi na ute wa mnyama aliyeambukizwa.
• Vilevile virusi hivi vyaweza kuenezwa kupitia vyombo, chakula, watu, hewa au hata ndege wa porini wenye virusi vya ugonjwa huu.
• Mayai yanayotagwa na kuku walioambukizwa yanaweza kuwa na virusi.
• Kuku kutoka eneo lenye ugonjwa kwenda eneo lisilo na ugonjwa
TIBA NA UDHIBITI:
• Kuweka uzio (Quarantine) na kuepuka uingizaji wa kuku walio na virusi ni njia
mojawapo ya kupunguza athari za mlipuko wa ugonjwa huu.
• Kusafi sha mabanda kila baada na kabla ya kuingiza kuku ili kuepusha maambukizi. Unaweza kutumia disinfenctant aina ya V-rid ambayo ina wigo mpana wa kuzuia maambukizi.
• Kuweka footbath kwa kutumia V-rid disinfectant
• Hakuna tiba ya ugonjwa huu, hivyo kuku wote wa eneo husika lazima wapate chanjo kila baada ya miezi mitatu au kama inavyoshauriwa
na wataalamu.
Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1
MFANO WA KUKU ALIYEKUFA KWA KIDERI
CHANJO:
Zipo aina nyingi za chanjo ya kideri
1. Kuna ya kuchanganya katika maji Newcastle disease vaccine Lasota strain
2. Kuna ya kupiga sindano Newcastle disease vaccine Hitchner strain (Ita new)
3. Kuna chanjo ya matone ya kuweka kwenye macho (I 2 Vaccine)
• Inapasa kumpatia kuku wako chanjo ya matone (I2) ambapo tone moja la dawa huwekwa kwenye jicho la kuku.
• Chanjo ya matone ya kwenye macho humpatia kuku kinga bora na ya muda mrefu kuliko ile inayotolewa kupitia maji ya kunywa. Kwa kutumia chanjo ya matone ya kwenye macho lazima itolewe kila baada ya miezi mitatu na itolewe pia kwa kuku wote wanaozaliwa katika
kipindi hicho na yapaswa wapatiwe chanjo haraka iwezekanavyo.
• Chanjo itolewe tu kwa kuku wasioambukizwa kideri na usijaribu kutoa chanjo kwa kuku walioambukizwa au kuomba kupatiwa chanjo wakati tayari kuna mlipuko wa ugonjwa huu. Ni vyema ukapata ushauri wa wanakijiji au wenyeji wa eneo husika kuhusu wakati ambao mlipuko wa kideri hutokea na kuweka mikakati ya chanjo inavyopasa. Pia inapasa kutoa chanjo mwezi mmoja au miwili kabla ya muda ambao mlipuko wa kideri unatarajiwa kutokea.
• Vilevile inapasa kufahamu kwamba chanjo ihifadhiwe kwenye sehemu yenye ubaridi na isiyo na mwanga.
• Inapasa kuelewa kwamba ugonjwa wa kideri husambaa haraka, hivyo ni muhimu kuzingatia kwamba kuku wote wa eneo husika wanapatiwa chanjo wakati mmoja. Kama mpango wa kutoa chanjo utafuatwa vyema basi kuna uwezekano kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huu. Hata hivyo kuku bado wanaweza kufa kwa magonjwa mengine kama kipindupindu cha kuku (Fowl cholera) na kadhalika.
ATHARI ZA UGONJWA WA KIDERI:
• Husababisha kupungua au kukosa kabisa nyama na mayai
• Vifo vya kuku.
• Kuongezeka kwa gharama za kudhibiti ugonjwa.
• Kupunguza kipato cha mfugaji.
Jifunze jinsi ya kumaliza tatizo la ndui kwa kuku ingia hapa link 1
HITIMISHO:
Ili kupunguza uwezekano wa mlipuko na maambukizi ya ugonjwa wa kideri mfugaji anashauriwa kuchanja kuku wake kama inavyotakiwa, kujenga banda bora la kuku na kuhakisha linakuwa safi wakati wote, kufungia kuku kwenye uzio wakati wa mchana ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa, kuhakikisha malishio na manywesheo ni safi wakati wote na kutoa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe kuku wanapoonyesha dalili za ugonjwa
Post a Comment