UNAANZAJE BIASHARA YA KUKU

 UNAANZAJE BIASHARA YA KUKU?


HOW TO START  UP FARMING POULTRY BUSSINESS

1.Chagua mbegu nzuri ili usipate shida kuuza.

2.Ujue mtaji wa kuku wako ili upange bei vizuri.

3.Fugia sehemu nzuri ili usipate upotevu wa kuku kabla hujaanza kuuza.

4.Pata uhakika wa soko kabla ya kuanza kufuga ili ujue utapeleka wapi wakikua.

5.Tambua wateja wakuu waliko ili uwafuate.


NAMNA YA KUTANGAZA BIASHARA YA KUKU

HOW TO PROMOTE BUSSINESS

1.Jenga Imani kwa wateja ili waifuate huduma ijitangaze yenyewe.

2.Tumia vyombo vya habari kufikia wateja wako.

3.Tangaza kupitia mitandao ya KIJAMII Chagua jina zuri la biashara yako na liwe la kipekee Tengeneza website za biashara yako.

4.Uza bidhaa yako na kusaidia huduma (giving back to the community).

5.Tafuta upekee uvutie kazi yako.


MAKOSA KATIKA UFUGAJI

1. Kuchagua mbegu bila kujua uhitaji wake.

2. Kutumia chakula cha nyama kwa kuku wa mayai.

3. Kufuga bila elimu ya kutosha.

4. Kununua kuku wageni na kuwaweka Banda moja na kuku waliokuwepo.

5. Kufuga bila malengo.

6. Kufuga bila kujipanga.

7. Kufuga bila kumbukumbu

8. Kufuga bila kujua masoko.

9. Kufuga bila kujua magonjwa,tiba,chanjo pamoja na kinga n.k.

UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA

Ni muhimu kuwa na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu 

Ili kumwezesha mjasiriamali kufuatilia gharama uzalishaji na uendeshwaji 

Kupata habari za masoko na bidhaa zako (kuku , vifaranga , mayai) 

1.Weka kumbukumbu ya kinachoingia na kutoka 

2.Weka kumbukumbu ya gharama za uzalishaji na uendeshaji 

3.Weka kumbukumbu ya aina ya bidhaa na wateja (customers)

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us