KANUNI ZA KUONGEZA FAIDA KATIKA UFUGAJI

KANUNI ZA KUONGEZA FAIDA KATIKA UFUGAJI


1.Kupata vifaranga bora , kuna baadhi ya kampuni uzalizalisha vifaranga visivyokuwa na afya bora 

Hivyo uchangia vifo vya kuku kwa asilimia kubwa a kutokana na magonjwa kutoka kiwandani , vile vile usababisha hasara kwa mnunuzi

2.Uleaji vifaranga , ni vema kuzingatia chanjoe zote , vile vile kuzingatia usafi bandani

3.Chakula bora , WAFUGAJI wengi ulalamika vifaranga kutokua vizuri , bila kutambua ubora wa chakula anachokula kuku

Kimsingi kuku anahitaji kupata chakula ambacho kina virutubisho vyote ikiwemo protein , vitamin , carbohydrates , fat and oil

4.Kupata soko la uhakika , ni vizuri mfugaji kuakikisha bidhaa yako baada ya kukamilika unaiuza wapi (improve productivity) 

Siku zote bidhaa yenye ubora ni laisi kufanya vizuri sokoni , 

JiNSI YA KUANZA BIASHARA YA UFUGAJI

1.Chagua aina ya kuku , unataka kuku wa kienyeji ! , Unataka kuku wa nyama ! , Unataka kuku wa mayai ! unataka kuku wa nyama na mayai ! 

2.Amua unataka kufuga kuku kwa malengo gani ! Pata lengo kuu la ufugaji (main objective purpose) uliza wafugaji wenzako ili uwe na taarifa kamili ya aina ya kuku

3.Una pesa za kotosha, lazima uhakikishe financial umejiandaa kuingia katika biashara , kwa maana ukubwa wa shamba lako unategemea na aina ya mtaji uliokua nao

4.Unatumia mfumo gani katika ufugaji wako wa kuku ! Huria , nusu huria , ndani , italaisisha bajeti yako ya chakula nk

5.Utawalisha nini kuku wako  , lazima ujue chanzo cha chakula cha kuku wako ili iwe laisi kucalculate gharama za chakula

6.Chanjo za kuku na Tina zake , lazima utambue kuwa ili kuku wawe na afya njema ni lazima uwe unawapa chanjo za magonjwa

SIMAMIZI MZURI WA CHAKULA CHA KUKU

• Wapatie kuku wako mlo kamili na kwa kiwango kinachowatosheleza na uwape nyongeza ya chakula kama vya majani, mifupa na magamba ya mayai.

• Hakikisha unawapatia maji safi wakati wote

• Safisha malishio na manywesheo kila siku hakikisha unayasugua na kusuuza vilivyo ili kuondoka utando unaoota kwa sehemu za ndani

ambazo kwa kawaida huhifadhi vijidudu hatarivya bakteria kama Salmonella na E. coli.

(Nunua nipples drinker)

• Nunua chakula chako kutoka msambazaji aliyethibitisha ili kuepuka uwezekano wa kuuziwa chakula kulichochafuliwa na sumu kuvu za Aflatoxin au salmonella na nyinginezo.

• Hifadhi chakula cha kuku kwenye sehemu kavu na baridi na usiache chakula ghalani zaidi ya miezi 3 kuepuka uwezekano wa kuzalisha sumu kuvu.

• Usilishe kuku wako chakula chochote ambacho kimeanza kutoa harufu ya uvundo au ukungu

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us