MFUGAJI JITAIDI KUFANYA HAYA KILA SIKU KUEPUKA MAGONJWA
1.Safisha vyombo vya chakula na maji kila kwa maji safi na salama
2.Safisha banda lako kila linapochafuka
3.Fata taratibu zote za chanjo (vaccination) kwa kuku wako
4.Weka utaratibu wa watu kuingia bandani (biosecurity)
Ikiwezekena kuwe na viatu ama sendo maalumu kwajili ya wageni wanaongia bandani kuepusha magonjwa ambukizi
5.Kaa bandani angalau dakika 5 au 10 kuangalia afya ya kuku zako , na ikiwa umeona dalili yoyote ya ugonjwa , mtenge kuku , na anza tiba mara moja
6.Epuka kuwapa chakula kilicho vunda (stunk food) uwa na bakteria wanaonweza kusababisha magonjwa
7.Kuku mgonjwa akifa , mzoga wake uchome moto ama mfukie sehemu ya mbali na mifugo yako
USAFI WA BANDA LA KUKU:
(A) Vyombo vya chalula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.
(B) Pumba au chakula kilicholowa na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolewe na kufukiwa.
(C) Choma moto/zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
(D) Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kama bata katika banda moja.
(E) Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
(F) Tumia dawa za kuulia vimelea kusafisha banda la kuku eg disinfectant
(G) Ziba matundu yote yanaweza kuruhusu panya na wanyama hatari kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
NB: Uwepo wa Banda bora , chakula bora, chanjo , ni muhimili wa kujikinga na magonjwa hatarishi kwa kuku
Post a Comment