FAIDA ZA KUWAPA KUKU MBOGAMBOGA AU MAJANI

 KUNA FAIDA KADHAA ZA KUWAPA KUKU MBOGAMBOGA  AU MAJANI


Tukianza na njia nzuri inayopendekezwa kitaalamu ni kuning'iniza mboga mboga au majani katika banda la kuku hii ni kwa wale kuku wanaofugwa ndani, pia unaweza kuyaning'iniza kwa nje sehemu unakowapaga chakula au kupumzikia hii kwa wale kuku wanaofugwa katika mazingira ya nje akiwepo kuku wa kienyeji.


Sababu kubwa ni kuzuia kudonoana, ulaji wa majani au mboga mboga huongeza vitamini A hasa unapowapa ikiwa bado mbichi bila kuanikwa maana ukianika unapunguza virutubisho.


Kutengeneza gamba la yai kwa wanaotaga (egg shell)

Mayai huwa na kiini cha njano.


Huzuia kuku kudonoana au kudonoa mayai


NB: Kuku wakizoea kupewa mboga za majani ukija kustop kuwapa inaweza kuwa sababu ya kudonoana au kudonoa mayai kwa kukosa walichokizoea.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

JE UNAMJUA  UMUHIMU WA VITAMIN NA MADINI YANAYOPATIKANA KWA KUKU?


UKOSEFU wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiria upungufu wa vitamin.


UMUHIMU WA VITAMINI.


Husaidia katika ukuaji wa kuku.


Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka.


Husaidia kuku kuwa mwenye afya.


Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri.


UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU.


Ukosefu wa vtamin 'A' hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin 'A' kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa ukosefu wa vitamun 'A' pia hata kuku wakubwa pia huathirika.


DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU.


Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji.


Hudhoofika na hatimaye kufa.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

TIBA NA KINGA


Kinga ya ugonjwa huu ni kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani

Wape kuku vitamini za kuku za dukani wakati majani hayapatikani kwa urahisi.


Kwa kuku alie athirika na ugonjwa huu msafishe na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi kasha pinya sehemu ya jicho na kutoa uchafu wote kasha msafishe, hakikisha uchafu wote unatoka kisha mpe vitamin ya dukani, fanya zoezi hilo kwa siku 5.


DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMINI B.


Manyoya huonekana kusambaratika, panga za kuku kuonekana zikiwa zimepauka, na kwa kuku watagaji hupunguza uwezo wao wa kutotoa mayai


JINSI YA KUKABILIANA NA JAMBO HILI.


Wapatie kuku wako Dawa za multivitamin.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN E.


Hizi ni dalili za ukosefu wa vitamin E kwa kuku,

Shingo kupinda kama kuku mwenye kideri.


Vifaranga huanguka kifudi fudi.


Utagaji wa kuku hushuka kwa kiasi kikubwa.


DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN D.


Ukosefu wa vitamin D hupelekea tatizo la mifupa kuwa laini, na hali hii hupelekea mifupa kupinda pia magoti huvimba na hata midomo kuwa laini. Na hata ukuaji wa kuku huwa hafifu. Hii hutokana na aina ya madini ya calcium na fosiforus kutojengeka kwenye mifupa.


Kwa kuku watagaji hali hii hupeleka kwa kuku watagaji kutaga mayai yenye ganda laini.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us