Vipimo vya banda Bora la kuku

 VIPIMO VYA BANDA


BANDA LA KUKU WA MAYAI (LAYERS) NA CHOTARA.

Kwa muda wa majuma manne ya mwanzo eneo la mita mraba 1 au eneo la hatua moja linatosheleza vifaranga 16. Banda lenye eneo la mita mraba 16 linaweza kulea vifaranga 320 hadi majuma 4. Baada ya majuma manne ya umri, nafasi iongezwe, hii itategemea na aina ya kuku na njia itakayotumika katika ufugaji  

KANUNI

Mita moja mraba inachukua kuku 6 pure wa mayai...ila kwa kuku chotara kama sasso na kuroiler ni kuku 4-5

kwahiyo ukichukua

Urefu 13 ×Upana 7= 91m²

Kwahiyo 91m²× 6 idadi ya kuku kwa mita moja mraba = 546 kuku wanaotakiwa kuwepo bandani.

Apo nimekadiria mita moja mraba itachukua kuku 6.

Hili banda linatakiwa kuwa na sehemu ya kutagia/Nest box...ambapo chumba kimoja cha kutagia kinatakiwa kutumiwa na kuku 4-5 hivyo angalia idadi yako ya kuku na ufanye huo uwiano.

Banda linatakiwa liwe na sehemu ya mazoezi/perches

           Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1                                    

BANDA LA KUKU WA NYAMA (BROILERS).

KANUNI

~~ Je nitahitaji ukubwa gani kufuga kuku 1000???

 1m² =  10 kuku

   × =1000 kuku

10×=1000

×=1000/10

×=100m²

 Kwamba mita moja ya mraba kwa broiler inaweza chukua kuku 10 - 12....kwahiyo hesabu ya kawaida 

 Mita moja mraba ichukue kuku 10....na wewe una kuku elfu 1000...unachukua 1000 gawanya kwa 10...unapata mita mraba 100 

 Kwahiyo unaweza  kuamua kujenga banda lenye marefu ya mita 14 na mapana ya mita 7....inaweza kutosha kabisa kwa kuku elfu moja ila usigawe vyumba utapunguza nafasi

Je wajuaa....unaweza ukafuga kuku kwa muda wote bila kubadilisha maranda??

Jibu ni :NDIO

Nini ufanye....Hakikisha madirisha ya banda lako ni makubwa pande zote....au nusu ukuta nusu wavu kuruhusu mzunguko mkubwa wa hewa, hakikisha maranda yana ujazo wa sentimita 5 kwenda chini hasa ya mbao hayaloani haraka

Hakikisha vinywesheo vya maji kwa kuku vimekaa juu kidogo kulingana na ukubwa wa kuku ilii wasimwage mwage maji

Maranda yatifuliwe angalau Mara mbili kwa wiki kuruhusu unyevu kukauka

 Angalizo: kama hutaweza kufanya niliyoelekeza nivema kubadilisha maranda kama ilivo zoeleka ili ugonjwa wa coccidiosis usitokee

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

KUMBUKA.

Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;

Kuongeza uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche ,mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.

Vile vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

KUMBUKA UELEKEO WA BANDA LOLOTE LA MIFUGO NI MASHARIKI - MAGHARIBI

maana yake ukuta mdogo (upana) uwe ni magharibi na nashariki kakini ukuta mrefu anabao utakuwa na wavu uwe upande wa kusini na kasikazini.. ili kuepuka jua kuingia moja kwa moja kwenye banda linapotoka na kuzama

Soma na hii

Fanya haya ukiona kuku wako anaumwa gusa hapa 👉👉link1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us