Mwongozo wa uleaji wa vifaranga

 


Muongozo wa Uleaji wa Vifaranga wa Kienyeji/Nyama/Mayai pamoja na Chotara


Mfugaji ni vizuri ujiandae kupokea vifaranga kama ambavyo hua unajiandaa kupokea mtoto kabla ya kujifungua.


Maandalizi hayo ni kama yafuatayo


1. Baada ya ujenzi wa banda kukamilika, banda lifanyiwe usafi wiki mbili kabla ya kuingiza vifaranga.


2. Wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga, matandiko yaliyosafishwa kuondoa vumbi yawekwe bandani, na banda zima lipuliziwe dawa (disfectant). Hakikisha kimo cha matandiko ni angalau inch 3


3. Tengeneza bruda kwaajili ya kuzuia joto lisipotee na andaa vifaa vya maji, chakula na magazeti yatakayo tandikwa juu ya Matandazo ndani ya bruda kuwasaidia vifaranga kutofautisha chakula na matandazo.


N.B: Badilisha magazeti hayo kila unapoona yamechafuka ndani ya siku 3-4 za mwanzo ambao utakua mwisho wa matumizi.


4. Kabla vifaranga kuingi bandani, bruda lipashwe joto kwa masaa sita huku vifaa vya maji yenye glucose na vitamin vikiwa ndani ya bruda. 

Baada ya masaa hayo vifaranga waingizwe bandani na kuruhusiwa kunywa maji yenye glucose kwa masaa 2 mfululizo. 


5. Hakikisha Kuna joto la kutosha muda wote ndani ya bruda ili kuzuia ugonjwa wa vichomi (Pneumonia). Unaweza kutumia vyungu, bulb ya 100w, chemli au vifaa vingine vya umeme au gesi.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us

Most Popular

Popular Posts