UGONJWA WA MIGUU KWA KUKU(Bumble Foot Diseases)

 UGONJWA WA MIGUU KWA KUKU(Bumble Foot  Diseases)


Bumble Foot Disease ni ugonjwa unashambulia miguu ya kuku au ndege wengine haswaa ktk nyayo,vidole na ktk maungio ya miguu.Unasababishwa na bacteria aitwaye 'Staphylococcus' ambaye huingia kupitia majeraha/michubuko ktk unyayo au vidole na kusababisha maambukiz yanayopelekea nyayo/vidole/kifundo cha mguu na hata mguu mzma kuvimba,kuoza na kusababisha kuku,bata,kanga n.k kushindwa kutembea na hali hiyo hupelekea kusimama kwa uzalishaji.


CHANZO


Miguu hupasuka na kupata majeraha/michubuko kutokana na sababu zifuatazo

1:Kukanyaga ardhi ngumu yenye mawe,kokoto au changalawe.


2:Lishe mbovu.


-Uzito mkubwa (heavy weight) kwa kuku pia husababisha nyayo kupasuka.


3:Kukanyaga kinyesi kwa muda mrefu ambacho huganda chini ya unyayo na endapo kuku anaishi ktk mazingira yenye unyevu nyevu hupelekea nyayo/vidole kupasuka na kuoza hivyo kuwapa nafasi bacteria kupenya na maambukizi.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

 JINSI YA KUDHIBITI/TAHADHARI


1:Kuku wasiishi ktk sakafu kavu na ngumu lazma wawekewe nyasi kavu au maranda au mchanga mkavu ktk sakafu ya banda au nje wanaposhinda.


2:Maranda/nyasi au mchanga uwe mkavu muda wote na wawekewe vichanja au bembea kwa ajili ya kupumzikia ili wasikanyage chini mda wote.


  TIBA


1:Kuku aliyeathirika atengwe na wengine,mpasue kwa kutumia kiwembe unyayo,vidole au kifundo cha mguu kilichoathirika safisha na kwangua na pamba au kitambaa safi kisha loweka miguu ktk maji ya uvugu vugu yenye chumvi kwa dakika 15 - 20 ili sehemu iliyoathirika ilainike, kausha miguu kisha safisha kwa kutumia hydrogen peroxide.

Soma zaidi

Mbinu za kutibu mafua ya kuku kwa haraka gusa hapa link 1

Post a Comment

Previous Post Next Post

Beauty

3/Beauty/post-per-tag

Labels

Nature

3/Nature/post-grid

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Facebook

Subscribe Us

Most Popular

Popular Posts